Afrika Kusini yaongeza wiki 2 watu kukaa ndani

0
817

Kufuatia kuendelea kuwepo kwa wagonjwa wa Corona nchini Afrika Kusini na virusi hivyo kuendelea kusambaa, Rais Cyril Ramaphosa ameongeza muda wa wananchi kuendelea kukaa ndani kwa wiki mbili (lockdown).

Shughuli zote zilifungwa nchini humo kwa kipindi cha wiki mbili na watu kutegemea kuendelea na shughuli zao za kila siku wiki ijayo, lakini serikali ya nchi hiyo imeona ni vyema watu wakaendelea kukaa nyumbani.

Nchi hiyo imezuia mikusanyiko ya watu, kufanya mazoezi ya kutembea/ kukimbia nje, uuzaji wa pombe na sigara, na misiba kuhudhuriwa na watu mwisho 50.

Hadi kufikia sasa nchi hiyo inayoongoza kuwa na wagonjwa wengi zaidi Afrika ina visa vilivyothibitishwa zaidi ya 1900 ikiwemo vifo 18.