Wananchi Mara kupunguziwa adha ya umbali wa kuitafuta elimu

0
176

Wananchi wa vijiji vya Nyatwali , Serengeti na Tamau mkoani Mara, wameomba kukamilishiwa ujenzi wa shule ya sekondari Nyatwali ili kuwapunguzia umbali wa kutembea zaidi ya kilomita thelathini kwa siku

Ombi hilo limetolewa na wananchi wa kijiji cha Serengeti wakati wakizungumza na mwandishi wa TBC mkoani humo.

Mkuu wa wilaya bunda Lydia Bupilipili akipokea saruji mifuko mia nne kutoka kwa mdau wa maendeleo mwanza huduma amesema msaada huo utasaidia katika kuboresha miundombinu ya shule

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda Justine Rukaka  amesema chama kitaendelea kuunga mkono juhudi  za wadau wa maendeleo nchini.