Muigizaji wa Star Wars ambaye pia ameshawai kufanya kazi na watu mashuhuri amefariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya corona (COVID-19).
Jill McCullough ambaye ni wakala wa muigizaji huyo amesema kuwa Andrew Jack mwenye umri wa miaka 76 amefariki akiwa katika Hospitali ya Surrey, nchini Uingereza
McCullough ameongeza kuwa Jack hakuweza kumuona mkewe katika siku zake za mwisho kwa sababu alikuwa amewekwa karantini kutokana na maambukizi ya virusi hivyo.
Miongoni mwa filamu zake za mwisho kabla ya umauti kumkuta ni pamoja na The Last Jedi na the Force Awakens.