Visa vya Corona Kenya vyafika 110

0
412

Idadi ya visa vya waathirika wa virusi vya corona nchini Kenya imefikia 29 baada ya kutangazwa kwa visa vipya 29 leo.

Visa hivyo vimefika 110 kutoka 89 viliyotangazwa jana Aprili Mosi na waziri wa afya wa nchi hiyo.

Wakati idadi ya waathirika ikiongezeka Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema kuwa idadi ya vifo nayo imeongezeka kufikia watu watatu.

Kiongozi huyo amesema kuwa serikali itachukua hatua kali zaidi kuhakikisha kuwa virusi hivyo havisambai zaidi.