Muathirika wa corona Tanzania afariki dunia

0
317

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza kuwa mmoja wa waathirika 19 wa virusi vya corona nchini Tanzania amefariki dunia alfajiri leo Machi 31,2020 katika kituo cha matibabu cha Mloganzila, Dar es Salaam.

Waziri amesema kuwa marehemu ni Mtanzania, mwanaume mwenye umri wa miaka 49, ambaye alikuwa akusumbuliwa na maradhi mengine.

Hadi leo asubuhi jumla ya watu waliothibitika kuugua homa ya mapafu inayosababishwa ni virusi hivyo ni 19, ambapo mmoja amepona na mmoja amefariki.