Libya imetangaza kuwaachia huru zaidi ya wafungwa 400 ikiwa ni hatua ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Uamuzi huo unafuatia hatua zilizochukuliwa na nchi nyingine zikiwemo Bahrain, Misri, Syria na Iran ambazo zimewaachia huru wafungwa kadhaa ili kujiepusha na maambukizi ya virusi hivyo vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 35,000 duniani.
Hivi karibuni Saudi Arabia ilitangaza kuwaachia huru wafungwa wapatao 250 ambao walikuwa wakitumikia vifungo kutokana na makossa madogo.
Hata hivyo hatua hiyo imekosolewa kutokana na wafungwa wa kisiasa na wale wanaotumikia vifungo kwa makosa mazito kutohusishwa katika msamaha huo.
Vikundi vya kutetea haki za binadamu na ndugu na jamaa wa wafungwa hao wametoa wito kutaka kundi hilo nalo pia linufaike na msamaha huo.