Corona: Serikali yaagiza tahadhari ichukuliwe kwenye minada ya samaki

0
238

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewaagiza viongozi wa serikali za mitaa kutokufunga minada pamoja na mialo ya samaki na badala yake wachukue tahadhari zaidi dhidi ya virusi vya corona.

Ulega amesema hayo alipokuwa akizungumza katika mnada wa Pugu, jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa serikali inataka kuona wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, lakini lazima tahadhari ichukuliwe ili kuhakikisha virusi hivyo havisambai.

Nao baadhi ya wafanyabiashara mnadani hapo wamesema wamekuwa wakifanya biashara zao katika tahadhari kuwa kwa kuhakikisha kila mmoja anafuata masharti ya kujikinga na virusi vya hivyo vinavyosababisha hom ya mapafu.

Aidha, Ulega ametembelea soko la samaki la feri ambapo ameeleza kuridhishwa na tahadahari zinazochukuliwa katika kupambana na virusi vya corona.