Klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania imefikia uamuzi wa kukata sehemu ya mishahara ya wachezaji na watumishi wa klabu hiyo, ili kusaidia katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.
Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa kikao cha bodi ya wakurugenzi kilichoendeshwa kwa njia ya video, kimefikia uamuzi huo ambapo tayari wachezaji na watumishi hao wameridhia.
Klabu hiyo pia imeamua kutoa majengo pamoja na maeneo kadhaa inayoyamiliki kwa serikali ya jimbo la Katalunya ili yatumiwe na idara ya afya ya jimbo hilo katika mapambano dhidi ya corona.
Hispania ni nchi ya pili kuathirika zaidi na virusi vya corona barani Ulaya baada ya Italia, ambapo hadi sasa watu elfu 56 wameambukizwa virusi hivyo na wengine takribani elfu nne wamefariki dunia.