Marekani yaizidi China kwa idadi ya waathirika wa corona

0
635

Wakati China ambayo ni kiini cha homa ya mapafu (COVID-19) ikiendelea kupambana vikali na virusi hivyo, Marekani imezidi kuathirika zaidi kwa kuwa na visa vingi kuliko sehemu nyingine yeyote duniani.

Takwimu za hadi leo Machi 27 zinaonesha kuwa kuna visa 85, 612 vya COVID-19 nchini Marekani, visa 81, 340 China, visa 80, 589 kutoka Italia, 57, 786 kutoka Hispania na Ujerumani ikishika nafasi ya tano kwa visa 47, 278.

Ingawa Marekani inaongoza kwa visa vilivyothibitishwa, Italia inaongoza zaidi kwa vifo vitokanavyo na virusi hivyo, ikiwa na vifo 8, 215, ikifuatiwa na Hispania yenye vifo 4, 365, kisha China yenye vifo 3, 292, Iran ikiwa na vifo 2, 234 na Marekani ina vifo 1, 301.

Nchi zinazoongoza kwa wagonjwa kupona ni China 74, 588, Iran 10,457, Italia 10, 361, Hispania ikiwa na wagonjwa waliopona 7, 015 na Marekani ikiwa na watu 1, 868 waliopona.

Hadi kufikia leo, Tanzania in visa 13. Takwimu zote zimetolewa katika ripoti ya corona.tuply.co.za