Uchaguzi mkuu uko pale pale: Rais Magufuli

0
276

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema virusi vya Corona havitazuia Tanzania kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Rais Magufuli amesema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa, kwa kuwa hakuna mtu anayependa kukaa ofisini muda mrefu.

“Hatujazuiliwa kukutana. Leo nimesoma gazeti moja linasema ‘Madiwani wafanya kikao,’ sijui alifikiri vikao vimezuiliwa sababu ya [virusi vya] corona. Sisi tunaendelea kukutana, hata bunge ndio maana linaendelea. Hata nchi zilizoathiriwa mabunge yao hayajafungwa,”amesema Rais Magufuli.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika halfa ya kukabidhiwa ripoti ya ukaguzi iliyoandaliwa na ofisi ya Madhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, pamoja na ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.