Waziri Mkuu akanusha taarifa za shule na vyuo kufunguliwa leo

0
261

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba shule na vyuo nchini vitafunguliwa hii leo si za kweli.
 
Amesisitiza kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji na zinapaswa kupuuzwa.
 
Machi 17 mwaka huu Waziri Mkuu Majaliwa alitangaza kuwa shule zote za awali, msingi na sekondari zitafungwa kwa muda wa siku 30 kufuatia mlipuko wa virusi vya corona nchini, na machi 18 alitangaza kwamba vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu navyo vitafungwa kwa muda wa siku 30.