Kanisa la EAGT laweka kambi kuliombea Taifa na janga la Corona

0
172

Kanisa la EAGT City Centre la Mtoni Mtongani limehitimisha maombi pamoja na funga kwa siku tatu ikiwa ni hatua ya kanisa hilo kuliombea Taifa kuepukana na Ugonjwa wa Corona.

Kambi hiyo ya siku tatu ilianza Ijumaa ya Machi 19 na kuhitimishwa leo Jumapili ambapo waumini wa kanisa hilo wamefanya sala pamoja na kufunga kula kwa ajili ya maombi hayo maalumu.

maombi hayo ya siku tatu bila kula wala kunywa yameambatanishwa na sadaka ili  kuliombea Taifa la Tanzania dhidi ya maangamizi ya virusi vya COVID 19.

Mchungaji Mkuu wa kanisa hilo  Florian Katunzi amesema kama wanaasayansi nguli duniani hawana ufumbuzi wa virusi vya korona basi Mungu awe ndio suluhisho la Mwisho.

Mchungaji Katunzi amemuomba Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dtk John Magufuli na watanzania kuendelea kumuomba Mungu na kutoa Sadaka ili kulinusu taifa na maradhi hayo.

Mchungaji Katunzi amesema lazima kuomba afya na kupona juu ya nchi na watu wake kama bibilia invyosema Zaburi 127:1