Idadi ya wanaougua corona yafikia 12

0
351

Serikali imesema kuwa hadi sasa watu Kumi na wawili wamethibitika kuugua homa ya corona.

Akilihutubia Taifa, Rais John Magufuli amesema kuwa, kati ya wagonjwa hao wanne ni raia wa kigeni na nane ni raia wa Tanzania.

Amesema wagonjwa wote isipokuwa mmoja, wametoka kwenye nchi zilizokuwa zimebainika kuwa na maambukizi ya homa ya corona.

Hata hivyo Rais Magufuli amewaeleza Watanzania kuwa wagonjwa wote wanaendelea vizuri na mpaka sasa hakuna kifo chochote kutokana na homa hiyo ya corona.

Amesema kuwa vipimo vyote vya leo vinaonyesha hakuna aliyekutwa na maambukizi na hata mgonjwa wa kwanza kugundulika na virusi vya corona, vipimo vimeonyesha hana ugonjwa huo.