Aurlus Mabele afariki dunia

0
1686

Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya Soukous,- Aurlus Mabele amefariki dunia jijini Paris nchini Ufaransa.

Taarifa za kifo cha mwanamuziki huyo mkongwe zimetolewa na msanii mwenzake wa kundi la muziki la Loketo, Nyboma Mwandido.

Aurlus Mabele ambaye alikua mtunzi na mwimbaji, alizaliwa mwaka 1953 katika wilaya ya Poto – Poto huko Congo Brazzaville.