Ligi Kuu Tanzania kuchezwa bila mashabiki

0
1692

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa, baada ya siku 30 serikali itakaporuhusu michezo kuendelea, itachezwa bila kuwa na mashabiki.

Azimio hilo limefikiwa na kikao cha Kamati ya Uongozi ya TFF kilichokutana leo ambapo imeeleza kuwa mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zitachezwa bila watazamaji, ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya #Corona.

Azimio hilo limekuja siku moja baada ya serikali kusitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwa ni sehemu ya hatua zilizochukuliwa kudhibiti maambukizi mapya ya virusi hivyo.