Hoteli aliyofikia muathirika wa Corona yafungwa, wahudumu wapimwa

0
328

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema tayari wataalamu wa afya wamechukua vipimo vya wafanyakazi wa hoteli alikofikia mgonjwa aliyegundulika kuwa na virusi vya corona, ili kubaini iwapo wamepata maambukizi au la.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Gambo amesema mbali na kuwapima wahudumu pia wameifunga hoteli hiyo.

Amewataka wakazi wa mkoa huo kuwa watulivu kwa kuwa tayari jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.