Raia wa Kenya kutosafiri nje kwa siku thelathini

0
498

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuzuia Raia wa nchi hiyo kusafiri nje ya nchi kwa muda wa siku thelathini kuanzia hii leo, ikiwa ni moja ya njia ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.


Akilihutubia Taifa, Rais Kenyatta amesema kuwa mpaka sasa watu watatu wamethibitika kuwa na virusi vya corona nchini Kenya, hivyo lazima ikaandaliwa mikakati ya dharura ya kukabiliana na virusi hivyo.


Amesema kwa wageni ambao tayari wameingia nchini huo, wanalazimika kutengwa kwa muda wa siku 14 ili kuona kama wameambukizwa virusi vya corona.


Rais Kenyatta ameagiza kusimamishwa kwa masomo katika taasisi zote za elimu nchini humo, ambapo shule za msingi pamoja zile za sekondari zitafungwa kuanzia hapo kesho.
Kwa upande wa vyuo vikuu, Rais Kenyatta ameagiza vyote viwe vimefungwa ifikapo machi Ishirini mwaka huu.