Baraza la wafanyakazi wa NEC lakutana

2
293

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekumbushwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu, ili kutimiza azma yake ya kufanya uchaguzi wa haki, uhuru na uwazi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani, Theresia Mmbando wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa NEC uliofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sylvius Mkwera amewataka watumishi wa tume hiyo kutumia mkutano huo kutafakari utendaji kazi wa taasisi hiyo.

Kwa upande wake Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) anayehusika na elimu kwa umma mkoani Pwani, Fredrick Mbigili amesema kuwa Idara yake itahakikisha vitendo vya rushwa vinadhibitiwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya kwanza na inajiandaa kuweka wazi daftari la awali na kuanza uboreshaji wa awamu ya pili hivi karibuni.

2 COMMENTS

Comments are closed.