Wasanii wa kike watakiwa kuzingatia maadili

0
1685
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza amesema serikali itazidi kuhakikisha mazingira ya kazi za sanaa yanakuwa rafiki.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza amewataka wanamuziki wa kike kuzingatia maadili na kufuata taratibu za nchi katika kufanya shughuli za muziki.

Shonza ameyasema hayo alipokuwa akizindua EP Album ya mwanamuziki Lulu Diva “The 4 Some” iliyozinduliwa usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Aidha, ameongeza kuwa serikali ipo bega kwa bega na wasanii kuhakikisha mazingira ya kazi za sanaa yanakuwa rafiki na kuwanufaisha kwa kazi zao.

Kwa upande wake Lulu Diva ameishukuru serikali kwa kuendelea kudhibiti mianya ya maharamia wa kazi za sanaa na kuahidi kuzingatia maadili ili kuwa mfano kwa wasanii wengine.

EP Album ya Lulu Diva, “The 4 Some,” ina jumla ya nyimbo nne, ambapo amewashirikisha wasanii mbalimbali kama vile Eddy Kenzo kutoka Uganda na Kaligraph wa nchini Kenya.