Bodi ya ligi kuu ya England yakutana

0
1470

Bodi ya ligi kuu ya England, inakutana na wakuu wa klabu zote za ligi hiyo ili kuona kama wanaweza kusimamisha au kuendelea na ligi hiyo kutokana na tatizo la ugonjwa wa corona kuwakumba baadhi ya wachezaji na kocha wa Arsenal, Mikael Arteta.

Tayari baadhi ya ligi mbalimbali barani Ulaya zimesimama lakini bado ligi kuu ya England inaendelea ingawa mchezo wa juzi kati ya Arsenal na Manchester City ulifutiliwa mbali kutokana na tatizo hilo la Corona.

Tayari kocha wa Arsenal, Mikael Arteta amewekwa kwenye karantini pamoja na wachezaji wake sawa na mchezaji wa Chelsea  Callum Hudson-Odoi na wachezaji wengine na benchi zima la ufundi la Chelsea nalo liko kwenye karantini.

Kikao cha leo baina ya Bodi ya ligi ya England na vilabu utaamua kama ligi hiyo isimame au iendelee

Katika hatua nyingine serikali ya Uingereza inafikiria kuzuia shughuli zote za kimichezo kutokana na tatizo hilo la Corona na waziri mkuu wa Uingereza, Moris Johnson anasema watachelewa kuchukua hatua hiyo lakini kama tatizo litazidi basi wanafikiria kuzuia