Sheria iliyotumika miaka 23 kufanyiwa marekebisho

0
324


 
Serikali inatarajia kuifanyia marekebisho sheria ya uwekezaji iliyotumika kwa zaidi ya miaka ishirini na mitatu,  ili iweze kuendana na mazingira ya sasa.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Anjela Kairuki,  mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa pamoja kati ya Wawekezaji kutoka Sweden na nchi za Afrika Mashariki, ufunguzi alioufanya kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza kwa niaba ya waratibu wa mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt Wilbroad Slaa amesema kuwa wawekezaji kutoka nchi za Scandnavia wamevutiwa kuwekeza kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na mazingira bora yaliyowekwa hivi sasa.

Ameongeza kuwa kuendelea kuboreshwa na kurahisishwa kwa mifumo ya uwekezaji pamoja na maboresho hayo kuwekewa mazingira ya kisheria, ni miongoni mwa maombi yanayowasilishwa na wawekezaji wengi wa nchi hizo za Scandnavia.