Chuo Kikuu Huria chashauriwa kutanua udahili

0
394

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameushauri uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Tume ya Vyuo Vikuu nchini kuhakikisha udahili wa chuo hicho unatanuliwa, kwa kuwa hadi sasa kuna kozi moja pekee ya maandalizi kwa ajili ya kuwaandaa vijana kuingia kwenye Shahada. 

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa ushauri huo katika mahafali ya 38 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, mahafali yaliyofanyika katika uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

Amesema katika kuongeza udahili kwenye elimu ya juu, ni vema Chuo hicho Kikuu Huria cha Tanzania kikawa na kozi ama programu za maandalizi kwa wale wanaotaka kusoma stashahada na kwa wale wa cheti pia na kwamba matokeo ya programu hizo yataongeza ushiriki wa Watanzania kwenye elimu ya juu.

Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 698 wametunikiwa vyeti katika ngazi mbalimbali