Mbio za Mwenge wa Uhuru mbioni kuzinduliwa

0
799

Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud amesema kuwa mkoa huo upo tayari kupokea ugeni utakaofika mkoani humo kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu zitakazofanyika Aprili pili.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja,  Ayoub Mohamed Mahmoud amesema  kuwa tayari maadalizi ya shughuli hiyo yameshaanza,  ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jukwaa kwenye eneo wa Mwehe, Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza kuchangia vifaa vya ujenzi,  ili kukamilisha ujenzi wa jukwaa hilo pamoja na barabara katika eneo hilo.