Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee, Esther Matiko wa Tarime Mjini na Ester Bulaya wa Bunda Mjini wote kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wametoka katika gereza la Segerea lililopo jijini Dar es salaam baada ya kukamilisha taratibu za kulipa faini ya jumla ya shilingi milioni 110 .
Hivi karibuni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwahukumu kulipa faini ya jumla ya shilingi milioni 350 au kifungo cha miezi mitano kwa kila kosa viongozi waandamizi wa CHADEMA pamoja na aliyekua Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt Vicent Mashinji baada ya kuwakuta na hatia katika makosa kumi na mawili.
Katika faini hiyo Mdee alitakiwa kulipa shilingi milioni arobaini, Bulaya shilingi milioni arobaini na Matiko shilingi milioni 30.