Mahakama yaombwa kutupilia mbali maombi ya Rugemarila

0
320

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara James Rugemarila, umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Dar es salaam kutupilia mbali maombi ya kuondolewa kwenye shauri hilo kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Maombi hayo yamewasilishwa na wakili wa serikali, -Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Huruma Shaidi, ambapo amedai kuwa pingamizi na maombi yamewasilishwa katika wakati usio muafaka kusikilizwa.

Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na wenzake wawili, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Machi 26 mwaka huu ambapo Mahakama hiyo itaitolea uamuzi.