Corona ni janga : WHO

0
431

Kwa mara ya kwanza Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza virusi vya corona kuwa ni janga.

Katika taarifa yake ya hivi karibuni WHO imesema kuwa, katika siku chache zijazo kutaripotiwa idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi hivyo , vifo pamoja na idadi kubwa ya nchi zilizoathiriwa na virusi hivyo vya corona.

Shirika hilo la Afya Duniani limefafanua kuwa huenda watu wengi katika mataifa mbalimbali duniani wakaambukizwa virusi vya corona duniani, kwa kuwa hawana kinga dhidi ya virusi hivyo.

Limesema linafuatilia kwa karibu mwenendo wa virusi hivyo, na hatua zinazochukuliwa kwa lengo la kukabiliana navyo.

WHO imetolea mfano nchi ya Marekani ambapo hadi sasa zaidi ya watu elfu moja wameambukizwa virusi vya corona, huku zoezi la kuwatambua wengine likiendelea, hali inayoashiria watu wengi zaidi watakua wameambukizwa.