Serikali yasisitiza kuendelea kuchukuliwa kwa tahadhari dhidi ya corona

0
176

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameziagiza taasisi zote nchini kuweka maji chirizi kando ya mashine za kuweka saini wakati wa kuingia na kutoka kazini, na sehemu zote za mashine za kutolea fedha ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Waziri Ummy amesema hayo jijini Dar es salaam katika mahojiano maalum na mwandishi wa TBC na kusisitiza kuwa Tanzania haina mtu yoyote aliyebainika kuwa na virusi vya corona lakini tahadhari ni muhimu ikachukuliwa.

Mpaka sasa virusi vya corona vimekwishaenea katika nchi 109 duniani.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka jamii kubadili tabia, utamaduni na mazoea na kuchukua tahadhari zinazotolewa na watalaam wa afya ili kujikinga na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.