Utalii wa twiga weupe Kenya watikisika

0
484

Wawindaji haramu wamevamia hifadhi ya kijamii ya Ishaqbini Hirola iliyopo Garissa, Kenya na kuuwa twiga mweupe na mwanae.

Twiga hao adimu hupatikana Kenya pekee Duniani kote. Kati ya twiga watatu waliokuwepo kwenye hifadhi hiyo, wawindaji walimuacha twiga dume mmoja ambaye pia alikuwa mtoto wa twiga aliyeuawa.

Wanakijiji pamoja na mgambo wa pori wamethibitisha kupatikana kwa miili hiyo miwili huku wakiomba wanakijiji kushirikiana katika kuhakikisha wanalinda wanyama adimu katika hifadhi zao.

Twiga hawa weupe wamekuwa sehemu kubwa ya utalii nchini Kenya katika kipindi cha mwaka 2017.