Waziri Mkuu atembelea makaburi ya Kola, atoa agizo

0
178

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea makaburi ya Kola yaliyopo katika manispaa ya Morogoro eneo walipozikwa marehemu wa ajali ya moto iliyotokea Agosti Kumi mwaka 2019, kwa lengo la kukagua ujenzi wa uzio kwenye eneo hilo.

Akiwa katika makaburi hayo, Waziri Mkuu emeeleza kuridhishwa na ujenzi huo huku akiuagiza uongozi wa mkoa wa Morogoro kuendelea kuboresha eneo hilo ili liendelee kuwa historia kwa vizazi vijavyo.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza fedha zitakazobaki katika ujenzi huo wa uzio kwenye makaburi ya Kola zitumike kuboresha eneo lote la makaburi.