Raia mmoja wa Thailand aliyepelekwa katika Hospitali ya Wilkins nchini Zimbabwe kwa ajili ya vipimo ili kubaini kama ana virusi vya corona ametoroka kabla ya kumaliza kupimwa.
Mtu huyo alikuwa amekwenda katika hospitali moja baada ya kuhisi kuwa ana homa, alipewa rufaa kwenda Wilkins ndipo alipolazimika kuanza kufanyiwa vipimo, lakini aliondoka bila ruhusa ya wauguzi, na haikubainika amekwenda wapi.
Wizara ya afya nchini humo imeeleza kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyethibitika kuwa na virusi hivyo.
Virusi hivyo viameanza kusambaa barani Afrika ambapo hadi sasa kuna visa 100, kama mgawanyiko unavyoonesha hapa chini:
Egypt – 55
Algeria – 20
Afrika Kusini – 7
Tunisia – 5
Senegal – 4
Morocco – 2
Cameroon – 2
Burkina Faso – 2
Nigeria – 2
Togo – 1