Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar e s salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi limebaini na kuthibitisha ndani ya mwili wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula kulikuwa na sumu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini sumu hiyo ilivyoingia mwilini mwake na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa kwa atayakebainika kuhusika na tukio hilo.