IMF yapongeza mabadiliko ya kisheria Tanzania

0
389

Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeipongeza Tanzania kutokana na mabadiliko yenye tija iliyofanya kwenye sekta ya madini, ardhi pamoja na huduma ndogo za fedha (microfinance), ambayo yamewezesha uchumi kukua.

Kutokana na mabadiliko yaliyofanywa hasa kubadili sheria ya madini yamesababisha mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa kupanda hadi asilimia 5 kutoka asilimia 4.8 mwaka uliopita. Wakati sekta ya madini ikizidi kutakata, hifadhi ya dhahabu na dola za kimarekani imekua kupita lengo la nchi, inatosha kwa kipindi cha miezi mitano.

Kwa upande wa mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini ya asilimia nne kwa takribani miezi 12, viwango vya kubadili fedha vikizidi kuwa imara, pamoja na kumarika kwa makusanyo ya fedha kufikia takribani asilimia 96 ya lengo.

Licha ya mabadiliko na mafanikio hayo, timu ya IMF ikiongozwa na Enrique Gelbard imeisihi Tanzania kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na mabadiliko ya kikodi ili kuhakikisha uchumi unaendelea kuimarika.