Simba yatobolewa tena mbele ya Rais Magufuli

0
455

Timu ya Simba leo imepoteza mchezo wake wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga katika mchezo wa kariakoo dabi uliopigwa dimba la Taifa Jijini Dar es salaam

Katika mchezo huo Simba imepoteza mchezo huo wa Kariakoo Dabi mbele ya Rais Magufuli na Rais wa CAF Ahmad Ahmad

Rais John Magufuli katika jukwaa la uwanja wa Taifa akishuhudia mechi ya Yanga na Simba

Bao pekee la Yanga limefungwa na mchezaji Bernard Morrison dakika ya 44 baada ya kuutandika vyema mkwaju wa adhabu ndogo uliomshinda golikipa Aishi Manula na kufanya wanajangwani kuondoka na furaha uwanjani hapo