Dkt. Abbasi: Uwanja wa Taifa urekebishwe ndani ya saa 12

0
425

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amewaagiza maafisa wa Wizara yake kusimamia haraka marekebisho ya eneo mojawapo la benchi la wachezaji wa akiba kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya kutoridhishwa na hali ya paa la benchi hilo.

Dkt. Abbasi amefika kukagua uwanja huo leo Jumamosi, uwanja utakaotumika kwa mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kesho Jumapili, ameeleza kuridhishwa na maandalizi ya uwanja huo lakini akashangaa eneo hilo la benchi kuwa na paa lililopasuka linaloweza kusababisha wachezaji wa akiba kulowa mvua ikinyesha.

Kutokana na hali hiyo, Dkt. Abbasi amewahoji watendaji wa Wizara hiyo aliokuwa nao na kisha kumpigia simu Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo na kumwagiza atoe fedha za marekebisho hayo leo.