Makamu wa Rais akagua maendeleo Hospitali Simiyu

0
215

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan leo amefanya ziara katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu akiongozana na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ili kujionea hali ya utoaji huduma za Afya katika hospitali hiyo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali Mpya ya Mkoa wa Simiyu Dk. Festo Dugange kuhusu Vifaa Vipya vilivyofungwa kwenye Hospitali hiyo leo wakati alipotembelea kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kiutendaji ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika Hospitali hiyo. kushoto Waziri wa afya Ummy Mwalimu.