Tetemeko jingine la ardhi limevitikisa visiwa vya Java na Bali nchini Indonesia zikiwa zimepita wiki mbili tuĀ tangu matetemeko mengine makubwa yalipoitikisa nchi hiyo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu elfu mbili.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi baada ya kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi, huku waokoaji wakiendelea na zoezi la kuwatafuta watu ambao hadi sasa hawajulikani walipo baada ya matetemeko hayo ya ardhi.
Matetemeko hayo ni tetemeko la kawaida la ardhi na tetemeko la ardhi chini ya bahariĀ – Tsunami.
Awali serikali ya Indonesia ilitangaza kuwa alhamisi wiki hii ndiyo ingekuwa siku ya mwisho ya kuendelea kuwatafuta watu ambao hawajulikani walipo, lakini waokoaji wameonyesha matumaini ya kuendelea kupata miili zaidi ya watu katika zoezi hilo.