Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, – Hamad Rashid Mohamed amesema kuwa, hakuna mtu yoyote aliyeingia visiwani humo na kugundulika kuwa na virusi vya corona.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja Waziri Hamad amesema kuwa, maafisa wa afya katika maeneo ya mikusanyiko ya watu ikiwa ni pamoja na bandarini na katika viwanja vya ndege wapo makini kufuatilia jambo hilo.
Aidha Waziri huyo wa Afya wa Zanzibar amesema kuwa, serikali inaunga mkono uamuzi wa ofisi ya Mufti wa kusitisha mkusanyiko wa Waumini wa dini ya kiislam kufika visiwani Zanzibar kwa ajili ya ibada ya IJITMAI iliyopangwa kuanza hii leo.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.