Afrika Kusini yatangaza kuwa na mgonjwa wa corona.

0
554

Raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 38 amethibitika kuwa na virusi vya corona.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imeeleza kuwa, katika siku za hivi karibuni mtu huyo akiwa na mke wake walisafiri na kwenda nchini Italia.

Mgonjwa huyo na mke wake ni miongoni mwa watu kumi waliowasili nchini Afrika Kusini Machi Mosi mwaka huu wakitokea Italia.