Nchi za SADC zatakiwa kuwa na mafunzo ya uzoefu wa kazi

0
665

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuiga mfano kwa Tanzania wa kuanzisha mpango wa mafunzo ya uzoefu wa kazi kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali,  ili kuwawezesha wahitimu hao kupata uzoefu kabla ya kuajiriwa.

Makamu wa Rais ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri na wadau wa sekta ya kazi na ajira wa nchi za SADC na kueleza kuwa imekuwa ni changamoto kubwa kwa vijana wanapoomba ajira na kukabiliwa na kikwazo cha kukosa uzoefu.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemevu Jenista  Mhagama amezitaka nchi Wanachama wa SADC  kutumia fursa ya uchumi wa viwanda zilizopo katika ukanda huo ili kutatua tatizo la ukosefu wa ajira.