Wakulima wa parachichi mkoani Iringa wamepata soko la uhakika la zao hilo baada ya kujitokeza mwekezaji ajulikanaye kama Kibidula Farm na kuanza kulima na kununua zao hilo na kisha kuuza nje ya nchi.
Mkuu wa mkoa huo wa Iringa, – Ally Hapi ametembelea shamba la mwekezaji huyo lililopo wilayani Mufindi na kuwataka Wakazi wa mkoa huo kutumia fursa hiyo kujiongezea kipato.