Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, – Ayoub Mohamed Mahamoud amewataka wanafunzi Visiwani Zanzibar kuzingatia elimu ili kutimiza ndoto zao na kuachana na matendo maovu.
Akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya Bububu, – Mahamoud amesema kuwa ni wajibu wa kila mwanafunzi kuongeza juhudi katika masomo yake kwa kuwa taifa linawategemea katika siku za baadaye.
Akiwa katika shule hiyo, pamoja na mambo mengine, Mkuu huyo wa mkoa wa Mjini Magharibi amekabidhi madawati na matofali kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani, vifaa vilivyotolewa na ofisi yake kwa lengo la kuunga mkono maendeleo ya sekta ya elimu.