Virusi vya Corona vyazidi kusambaa Afrika

0
552

Wakati dunia ikiendelea kupambana na virusi vya homa ya Corona, virusi hivyo vimenza kusambaa katika nchi mbalimbali za Afrika, hali inayozusha hofu miongoni mwa wananchi.

Wizara ya Afya ya Morocco, Machi 2 mwaka huu imethibitisha kuwapo kwa muathirika wa kwanza wa virusi hivyo nchini humo, ambaye ni raia wa nchi hiyo anayeishi nchini Italia.

Wakati hayo yakitokea, Tunisia na Senegal kwa nyakati tofauti zimetoa ripoti zinazoonesha kuwa kuna waathirika wa virusi vya corona. Mgonjwa aiyepo Tunisia ni raia wa Italia aliyewasili nchini humo kwa boti Februari 27, 2020, na mgonjwa aliyepo Senegal ni raia wa Ufaransa.

Kusambaa kwa virusi hivyo katika nchi za Afrika kunazua hofu kutokana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inayoonesha kuwa nchi nyingi za Afrika zina mifumo dhaifu ya kiafya kuweza kupambana na virusi hivyo kwa ufanisi.

Hadi sasa nchi za Afrika ambazo zimeripoti kuwemo muathirika wa virusi vya Corona ni Morocco, Tunisia, Senegal, Algeria, Nigeria, na Misri.