TBC yapongezwa kwa kuhamasisha Kiswahili fasaha

0
154

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameyashauri mabaraza ya kukuza Kiswahili Bakita na Bakiza kuratibu tafsiri za pamoja ya maneno ya Kiswahili ili kuondoa mkanganyiko katika matumizi yake.

Makamu wa Rais ameyasema hayo jijini DSM wakati wa mahojiano maalum na TBC, ambapo ameipongeza TBC kwa kazi wanayofanya ya kutangaza na kuhamasisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili.