Makamu wa Rais, mgeni rasmi kilele siku ya wanawake, kuzindua miradi mkoani Simiyu

0
228

Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani kitafanyika mkoani Simiyu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema maadhimisho hayo yatatanguliwa na maonesho ya wajasiriamali yatakayodumu kwa siku saba

Mtaka amesema pamoja na kuwa mgeni rasmi, Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa na ziara ambapo atazindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali mkoani humo

Maadhimisho wa siku ya wanawake duniani yanaendelea katika mikoa mbalimbali na kilele chake ni Machi 8 kauli mbiu ikiwa ni kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadaye.