Masauni: Ondoeni wakimbizi wahalifu makambini

0
198

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameviagiza Vyombo vya Ulinzi wilayani Kibondo mkoani Kigoma kuwaondoa makambini wakimbizi zaidi ya Elfu moja waliokamatwa nje ya makambi mkoani humo wakijihusisha na matendo ya uhalifu.

Masauni ametoa kauli hiyo wakati akiongea na wakimbizi kutoka nchini Burundi walioko katika Kambi ya Nduta wilayani Kibondo ambapo huku amewataka wakimbizi hao kuendelea kujiandikisha kurejea nchini kwao ambako amani imerejea.