Ronaldinho aingia matatizoni Paraguay

0
536

Mchezaji mkongwe wa Brazil na balozi wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania Ronaldo De Assis Moreira maarufu kama Ronaldinho Gaucho amejikuta matatizoni nchini Paraguay, baada ya kutuhumiwa kuingia nchini humo akiwa na hati bandia ya kusafiria.

Maafisa wa uhamiaji nchini Paraguay wamedai kuwa, Ronaldinho mwenye umri wa miaka 39 pamoja na Kaka yake kwa sasa wanashikiliwa katika hoteli moja nchini humo

Wamesema hati za kusafiria za Ronaldinho na kaka yake zina majina yao halisi pamoja na picha zao, lakini tatizo lililopo zinaonyesha wana uraia wa Paraguay kitu ambacho ni cha uongo.