Adhabu ya karipio yamshukia Kinana

0
412

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais John Magufuli, imeazimia kumpa kalipio Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho Abdulrahman Kinana kitokana na makosa yaliyokua yakimkabili.

Mbali na adhabu hiyo ya karipio, Kinana atakua chini ya uangalizi kwa muda usiopungua miezi 18.

Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Humphrey Polepole amewaambia Waandishi wa habari kuwa, katika kipindi hicho Kinana hataruhusiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi isipokua atakua na haki ya kupiga kura.