CCM yamsamehe Makamba

0
551

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemsamehe Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho Mzee Yusuf Makamba.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, – Humphrey Polepole amesema kuwa Makamba amesamehewa makosa yake kwa misingi kuwa amekua mtiifu na mnyenyekevu wakati wote alipoitwa kwa ajili ya mahojiano na pia ameomba asamehewe makosa yake kwa maandishi.