Samatta kuiongoza Aston Villa kuikabili Man City

0
501
Nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta.

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta anatarajia kuiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu yake ya Aston Villa itakapowavaa mabingwa watetezi wa Carabao Cup, Manchester City, Machi Mosi mwaka huu.

Aston Villa ilitinga fainali ya Carabao Cup baada ya kuiondoa Leicester City, huku Machester United ikiondolewa na Manchester City.

Mchezo wa fainali ya Carabao Cup utafanyika katika dimba la Wembley jijini London, uwanja wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 90,000.

Timu hizo mbili zinakutaka kuwania taji hilo wakati kila moja ikipambana kwa namna yake kwenye Ligi Kuu ya England. Wakati Man City ikipambana kuhakikisha ushindi ili iwakaribie mahasimu wao Liverpool, Aston Villa inapambana kuhakikisha kuwa haishuki daraja.