Lebanon kutatua mdororo wa uchumi

0
454

Serikali mpya  ya Lebanon imeanza kufanya jitihada za kuandaa rasimu ya mpango wa dharura wa kutatua mdororo wa uchumi nchini humo, ambao umekuwa ukisababisha maandamano yanayokuwa yakiambatana na ghasia.

Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo Hassan Diab amekuwa akijaribu kujadiliana na mataifa mbalimbali yanayoweza kuisaidia serikali yake kiuchumi, ili iweza kufufua uchumi na hatimaye kumaliza malalamiko ya waandamanaji.

Hata hivyo mataifa mengi wahisani yalionesha nia ya kuisaidia Lebanon, na kusema yatakuwa tayari kuisaidia nchi hiyo endapo serikali mpya iliyoko madarakani itaonesha utayari wa kufanya mabadiliko.

Mataifa hayo yamesema matakwa ya waandamanaji ni vema yakatekelezwa, ikiwa ni pamoja na yale ya kutaka kukomeshwa kwa vitendo vya rushwa katika ngazi mbalimbali za uongozi na udhibiti wa matumizi mabaya ya mali za umma.